Trump amekwenda kinyume na sera ya Marekani kuhusu Ukraine na Russia, na kupelekea majibizano katika white house wiki iliyopita, Trump aliposema kwamba rais wa Volodymyr Zelenskiy alikuwa hana shukran kwa msaada wa Washington.
Hatua ya Marekani kusitisha msaada kwa Ukraine inawashurutisha washirika wa Ulaya wakiongozwa na Uingereza na Ufaransa, ambao viongozi wao walifika white house wiki iliyopita, na wamemkumbatia Zelenskyy wazi wazi tangu alipoondoka White house.
Nchi za Ulaya zinachukua hatua kuimarisha ulinzi wao na kutoa msaada kwa Ukraine, ikiwemo kutafuta namna ya kumaliza vita, japo zinasema bado zinahitaji msaada wa Marekani.
Mkuu wa tume ya Umoja wa Ulaya Ursula Von der Leyen ametangaza mapendekezo ya kuongeza bajeti ya ulinzi ya Ulaya, ambayo anasema inahitaji dola bilioni 840.
Umoja wa Ulaya unatarajiwa kuandaa mkutano wa dharura Alhamisi, Machi 6.
Forum