Wizara ya ulinzi ya Russia imesema kuwa vikosi vyake vimekamata Sudne na Burlatske kusini mwa mkoa wa mashariki wa Donetsk.
Miji hiyo iko karibu na mji wa Velyka Novossilka, ambao ulishikiliwa na jeshi la Russia mwishoni mwa Januari.
Jeshi la wanaanga la Ukraine limesema Russia imerusha ndege 154 zisizo na rubani usiku, ambapo 103 kati yao zilitunguliwa na 51 kutoweka kwenye rada bila kusababisha uharibifu au hasara.
Mamlaka za eneo la Ukraine hata hivyo ziliripoti kifo kimoja na majeruhi kadhaa.
Katika eneo la kusini la Odesa, mtu mmoja alikufa na watatu walijeruhiwa, kulingana na waendesha mashtaka wa Ukraine.
Forum