Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Aprili 07, 2025 Local time: 09:02

Ramaphosa asema kumekuwa na ukosefu wa maelewano kati ya mataifa makubwa


Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa akihutubia Mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa G20, huko Afrika Kusini.
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa akihutubia Mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa G20, huko Afrika Kusini.

Mawaziri wa mambo ya nje wa nchi zenye Uchumi mkubwa - G20 wanakutana Afrika Kusini leo  Ijumaa kufuatia mivutano baina ya wajumbe kuhusu vita vya Ukraine na migogoro ya kibiashara.

Mawaziri wa mambo ya nje wa G20 wakutana Afrika Kusini.
Mawaziri wa mambo ya nje wa G20 wakutana Afrika Kusini.


Afrika Kusini inashikilia urais wa kundi hili, kwa Rais Cyril Ramaphosa kwa mara ya kwanza Mkutano wa G20 kufanyika Afrika imekuwa ni fursa kupata mataifa tajiri kuangalia wasiwasi wa mataifa masikini duniani.
Akizungumza wakati wa hotuba ya ufunguzi Ramaphosa alisema kumekuwa na ukosefu wa maelewano kati ya mataifa makubwa ikiwa ni Pamoja na G20 kuhusu jinsi ya kushughulikia maswala ya kimataifa.


Nchi za G20 zinazowakilisha baadhi ya asilimia 85 ya pato la taifa na robo tatu ya biashara mara nyingi zinapata shida kuonana macho kwa macho lakini mifarakano tangu Russia ilipoivamia ukraine mwaka 2022 imesababisha kuwepo na mikanganyiko kuliko hapo awali.

Forum

XS
SM
MD
LG