Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 12, 2024 Local time: 03:44

Familia za Syria zaendelea kuungana na wenzao walioachiliwa jela na waasi


Picha ya maktaba ya wafungwa wa Syria
Picha ya maktaba ya wafungwa wa Syria

Familia za wafungwa wa Syria Jumatatu zilikuwa zinazunguka kwenye vyumba vichafu katika jela ya Sednaya mjini Damascus  kujaribu kuona dalili za kuwpata jamaa zao waliofungwa kwa muda mrefu pale milango ilipofunguliwa na waasi.

Maelfu ya wafungwa waliondoka jela Jumapili baada ya kuangushwa kwa utawala wa Assad, baadhi wakiungana na jamaa zao, ambao kwa muda mrefu waliamini kuwa waliuwawa. Hata hivyo familia nyingi zinaendelea kuwatafuta watu wao ndani ya jela hiyo wengi wakiwa wamezuiliwa kutokana na kushiriki maandamano au kuupinga utawala wa Assad.

Mmoja wa wanafamilia waliofika kwenye jela hiyo ni Ahmed Najjar akitokea Aleppo akiwa na matumaini ya kuwapata watoto wa ndugu zake wawili, waliokamatwa na maafisa wa usalama wa Assad 2012. Amesema kuwa wanaendelea kuwasaka hadi kwenye vyumba vya chini ya ardhi. Uvumi uliokuwa ukienea Jumapili ni kwamba huenda kuna maelfu ya wafungwa waliopo kwenye jela iliyopo chini ya ardhi.

Hata hivyo kufikia Jumatatu jioni, hakukua na matumani ya kuwapata wafungwa zaidi. Makundi ya kutetea haki za binadamu yameorodhesha mauaji kwenye jela za Syria, wakati Marekani ikisema 2017 iligundua sehemu ya kuchoma miili ya watu ndani ya jela ya Sednaya, baada yao kunyongwa.

Forum

XS
SM
MD
LG