Papa Francis amepelekwa hospitali leo Ijumaa saa za asubuhi za Italia kwa ajili ya uchunguzi wa kiafya na kuendelea na matibabu ya ugonjwa wa bronchitis, Vatican imesema.
“Asubuhi ya leo, mwishoni mwa ibada yake, Papa Francis alilazwa katika hospitali ya Policlinico Agostino Gemelli kwa uchunguzi wa kina na kuendelea na matibabu yake ya ugonjwa wa bronchitis ambao bado unaendelea katika mazingira ya hospitali”, ilielezwa katika taarifa hiyo.
Papa Francis mwenye umri wa miaka 88 amekuwa Papa tangu mwaka 2013 na amekuwa akisumbuliwa na mafua pamoja na matatizo mengine ya kiafya mara kadhaa katika miaka miwili iliyopita.
Mapema mwezi huu, Francis aliwaambia mahujaji katika ibada ya kila wiki kwamba alikuwa akitaabika na mafua makali ambapo baadae ilielezewa na Vatican kuwa ni ugonjwa wa bronchitis.
Forum