Hatua hiyo ya Besigye ni kupinga kushikiliwa kwake jela ,mmoja wa mawakili wake aliliambia shirika la habari la AFP siku ya Alhamisi.
Wakili Erias Lukwago anasema walimtembelea akiwa jela jana lakini hali yake ya kiafya inatia wasiwasi. Anaumwa sana na anahitaji huduma za afya haraka.
Lukwago alitangaza jumatano kwamba Besigye alikuwa katika mgomo wa kula kupinga kufungwa kwake kinyume cha sheria na alikuwa anaumwa sana kiasi cha kushindwa kuhudhuria kesi mahakamani.
Wakati huohuo msemaji wa jela Frank Baine alikataa kuzungumzia kuhusu suala hilo lakini akaiambia AFP “ jengo letu lina vifaa vya kutosha kumuhudumia Besigye kama ilivyo kwa wafungwa wengine.”
Forum