Besigye alitekwa nyara mwezi novemba akiwa nchini Kenya na kurudishwa Uganda, alipofunguliwa mashtaka katika mahakama ya kijeshi, ya kumiliki bastola
Anakabiliwa na hukumu ya kifo endapo atapatikana na makosa ya kupanga njama yakupindua serikali.
Wakili wa Besigye Erias Luakwago, amesema kwamba Besigye, mwenye umri wa miaka 68, alianza mgomo wa kutokula Jumatatu wiki hii, kwa sababu anahisi hana lingine la kufanya kutafuta uhuru wake, kando na kukataa chakula akiwa kizuizini.
Mahaka ya kikatiba iliamua mwezi uliopita kwamba raia kama Besigye, hawastahili kufunguliwa kaesi katika mahakama ya kijeshi na raia wote ambao kesi zao zinasikiliwa na mahakama hiyo, wahamishiwe katika mahakama za kawaida kwa sababu mahakama za kijeshi hazina uhuru.
Hata hivyo, maafisa wa usalama wamekataa kumuachilia huru Besigye.
Forum