Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Machi 31, 2025 Local time: 04:38

Serikali ya Somalia inadai imewaua zaidi ya wanamgambo 70 wa Al-Shabaab


Kikosi cha jeshi la Somalia cha operesheni maalum
Kikosi cha jeshi la Somalia cha operesheni maalum

Zaidi ya wanamgambo 70 wa kundi la Al-Shabaab waliuawa nchini Somalia katika operesheni ya jeshi kwa ushirikiano na vikosi vya ndani, wizara ya habari ilisema Jumanne.

Kundi la Al-Shabaab lenye uhusiano na Al-Qaeda limekuwa likipambana na serikali kuu ya Somalia kwa zaidi ya miaka 15, kujaribu kuweka utawala wa sheria ya Kiislamu katika nchi hiyo maskini.

“Zaidi ya wanamgambo 70 wenye itikadi kali waliangamizwa katika juhudi za pamoja za jeshi la taifa na vikosi vya ndani,” wizara hiyo ilisema katika taarifa.

Operesheni hiyo ilifanyika Jumanne katika maeneo kadhaa ya jimbo la Hirshabelle, kusini mwa Somalia, wizara hiyo iliongeza.

Shirika la habari la AFP halikuweza kuthibitisha idadi hiyo ya vifo lakini mashahidi kadhaa wamethibitisha mapigano hayo.

Forum

XS
SM
MD
LG