Kiir aliwafuta kazi makamu wake wawili kati ya watano katika serikali yake ya umoja, na kumpandisha cheo mshirika wake Benjamin BoI MeI kuwa makamu wa rais anayesimamia wizara ya uchumi, katika amri ya rais iliyosomwa Jumatatu jioni kwenye televisheni ya taifa.
Alimfuta kazi pia Akech Tong, aliyeteuliwa mwezi Oktoba, kama mkuu wa usalama wa taifa. Amri hiyo haikutaja mrithi wa wadhifa huo. Amri hiyo haikueleza pia sababu za kufanya mabadiliko hayo.
Forum