Eneo la mashariki mwa DRC, ambalo limekumbwa na miongo kadhaa ya mzozo usiokoma, limetumbukia katika machafuko mapya baada ya waasi wa M23 kuteka maeneo makubwa katika majimbo ya Kivu Kaskazini na Kivu Kusini.
Katika mahojiano na shirika la habari la AFP wakati wa ziara yake mjini Kinshasa, mwendesha mashtaka wa ICC Karim Khan alikiri kushindwa kwa mfumo wa mahakama za kimataifa kukomesha ukatili wa kutisha ulioambatana na miongo kadhaa ya migogoro katika eneo hilo. Alisema “ana wasiwasi mkubwa kutokana na kuongezeka kwa machafuko”.
ICC ambayo iliwatia hatiani watu watatu kwa makosa ya ukatili mashariki mwa DRC, hivi sasa inachunguza uhalifu zaidi katika eneo hilo, “ikiangazia hadithi mbaya kutoka mashariki mwa Congo”, alisema.
Ameunga mkono pendekezo la serikali ya DRC kuunda mahakama maalum kwa ajili ya nchi hiyo, ambayo inatarajiwa kujadiliwa mwezi Aprili katika mkutano wa kimataifa mjini Kinshasa.
Forum