Mkuu wa masuala ya kibinadamu kwenye Umoja wa Mataifa ametoa wito kwa Jumuia ya kimataifa kuchukua hatua za haraka ili kushughulikia mzozo wa Sudan unaozidi kuwa mbaya, akisisitiza mateso kwa mamilioni ya watu waliokoseshwa makazi kutokana na mzozo huo.
Wanaharakati kutoka makundi mbalimbali ya mazingira ikiwa ni pamoja na Shirika la WWF na Greenpeace walikusanyika nje ya kituo cha maonyesho na mkutano wa mazingira mjini Busan wakitoa wito wa kupitishwa kwa mkataba wa plastiki wenye nguvu zaidi ili kukabili uchafuzi wa mazingira.
Chama cha upinzani nchini Namibia Alhamisi kimeomba zoezi la kuhesabu kura lisitishwe baada ya uchaguzi wa taifa kukabiliwa na changamoto za kiufundi na upigaji kura kuendelea baada ya muda wa kufungwa kwa vituo vya kupigia kura.
Vita vinavyoendelea nchini Sudan kwa mara nyingine vinajadiliwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, UN, kukiwa kuna rasimu ya azimio lililoandikwa na Uingereza.
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu Jumanne amemfukuza kazi Waziri wa Ulinzi Yoav Gallant kutokana na kutoaminiana wakati wa vita vya Gaza dhidi ya Hamas, ofisi yake imesema.
Waziri wa mambo ya kigeni wa Iran Abbas Araghchi, Jumatano amewasili mjini Cairo, Misri, ikiwa ziara ya kwanza ya waziri wa kigeni wa taifa lake kwa karibu miaka 12, chombo cha habari cha serikali kimesema.
Ajali ya basi kwenye barabara kuu nchini Misri iliua watu 12 na kujeruhi wengine 33 Jumatatu, wizara ya afya ya nchi hiyo ilisema katika taarifa.
Mamlaka ya kuendesha mashtaka nchini Afrika Kusini Alhamisi ilisema haitaendelea na mashtaka ya utakatishaji fedha na ufisadi dhidi ya Rais Cyril Ramaphosa yanayohusiana na wizi wa dola za Marekani uliofanyika kwenye shamba lake mwaka 2020.
Viongozi wa Misri, Eritrea na Somalia Alhamisi waliahidi kushirikiana pamoja juu ya usalama wa kikanda katika mkutano usio wa kawaida uliofanyika licha ya mivutano inayozidi kuongezeka katika Pembe ya Afrika.
Watu 893,000 wameathiriwa na mafuriko nchini Sudan Kusini na zaidi ya 241,000 kukoseshwa makazi, shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu misaada ya kibinadamu (OCHA) lilisema Alhamisi katika ripoti iliyosahihishwa kuhusu janga hilo.
Bei ya mafuta iliongezeka Jumatano kwenye vituo vya mafuta kote nchini Nigeria, likiwa pigo lingine kwa raia wa Nigeria ambao tayari wanakabiliwa na mzozo mbaya wa kiuchumi katika miongo kadhaa.
Kombora la masafa marefu la Russia kwenye bandari katika mkoa wa kusini mwa Ukraine wa Odesa liliua watu sita na kujeruhi wengine 11 Jumatano, maafisa walisema.
Makamu wa Rais wa Kenya Rigathi Gachagua Jumatatu alikanusha madai ya ufisadi dhidi yake katika mkesha wa kura ya kutokuwa na Imani naye ambayo inaashiria mgawanyiko mkubwa katika chama tawala.
Rais wa Tunisia aliye madarakani Kais Saied anatarajiwa kushinda uchaguzi wa rais nchini humo kwa asilimia 89.2 licha ya idadi ndogo ya wapiga kura, kulingana na matokeo ya awali yaliyotangazwa Jumapili kwenye televisheni ya taifa baada ya upigaji kura kumalizika.
Umoja wa Ulaya ulitoa msaada wa euro milioni 5.4 kwa nchi sita za Afrika Magharibi na Afrika ya Kati zilizokumbwa na mafuriko mabaya, ujumbe wa Umoja wa Ulaya nchini Chad ulisema Jumatano.
Waendesha mashtaka wa Benin Jumatano walisema kwamba watu watatu mashuhuri akiwemo kamanda wa kikosi cha ulinzi wa rais walikamatwa kwa tuhuma za kupanga “mapinduzi” katika taifa hilo dogo la Afrika Magharibi.
Mawaziri kadhaa wa zamani wa Mali na maafisa wakuu wa kijeshi walifikishwa mahakamani Jumanne kujibu tuhuma za kupora mamilioni ya dola wakati wa ununuzi wa ndege ya rais mwaka 2014 pamoja na zana za kijeshi.
Miezi mitatu baada ya maandamano makubwa dhidi ya serikali nchini Kenya, shirika la haki za binadamu Amnesty International linatarajiwa kuwasilisha ombi leo Jumatano ili kuundwe tume itakayochunguza vifo vya watu kadhaa kutokana na “polisi kutumia nguvu kupita kiasi kinyume cha sheria.”
Viongozi wakuu wa upinzani nchini Tanzania waliachiliwa Jumatatu jioni, chama chao kimesema, baada ya kushikiliwa na polisi ambao walizuia maandamano yaliyokuwa yamepangwa jijini Dar Es Salaam katika hatua ya hivi karibuni ya kuwanyamanzisha wapinzani.
Kundi la wanajihadi lenye uhusiano na Al-Qaeda Jumanne lilidai kuhusika na shambulizi baya katika mji mkuu wa Mali, Bamako, ambapo wapiganaji wa kundi hilo walidhibiti kwa muda sehemu ya uwanja wa ndege wa kimataifa.
Pandisha zaidi