“Kaimu mwanasheria mkuu James McHenry amechukua uamuzi huu kwa sababu hakuwa na imani kwamba maafisa hawa wanaweza kuaminiwa ili kutekekeza ajenda ya rais kwa uaminifu kwa sababu ya jukumu lao katika kumfungulia mashtaka rais,” afisa wa wizara hiyo alisema.
Afisa huyo hakufafanua ni watu wa ngapi waliofukuzwa, lakini vyombo vya habari vya Marekani vilisema ni zaidi ya watu 10 na wengi wao walikuwa waendesha mashtaka wanaofanya kazi kwenye wizara ya sheria.
Mwendesha mashtaka maalum Jack Smith, ambaye aliwasilisha kesi mbili dhidi ya Trump kwenye mahakama za serikali kuu, alijiuzulu mapema mwezi huu.
Forum