Wabunge nchini Gabon walikutana Alhamisi kuanza kujadili rasimu ya katibu mpya, hatua ya kwanza kuelekea kurejeshwa kwa serikali ya kiraia, ambayo utawala wa kijeshi uliahidi kufuatia mapinduzi ya 2023.
Rais wa Senegal Bassirou Diomaye Faye Alhamisi alitangaza kuwa amelivunja bunge linaloongozwa na upinzani na kuitisha uchaguzi mpya wa bunge tarehe 17 Novemba.
Mafuriko makubwa katika mji wa kaskazini mashariki mwa Nigeria yameua watu 30 na kulazimisha wengine 400,000 kuhama makazi yao, maafisa walisema Jumatano.
Wagombea wawili wa uchaguzi wa rais nchini Algeria ambao walishindwa na rais aliye madarakani Abdelmadjid Tebboune waliwasilisha rufaa kwenye Mahakama ya Katiba Jumanne, kupinga matokeo ya muda ya uchaguzi huo.
Takriban watu 18, wakiwemo raia wa kigeni, walifariki na wengine wanne kutoweka baada ya mafuriko kusini mwa Morocco, wizara ya mambo ya ndani ilisema Jumatatu, ikisahihisha idadi ya awali ya watu 11 waliokufa.
Mafuriko makubwa ya wiki kadhaa nchini Chad yamesababisha vifo vya watu 341 na wengine milioni 1.5 wameathirika tangu mwezi Julai, Umoja wa Mataifa ulisema Jumatatu.
Shambulizi la kombora katika soko la Sennar kusini mashariki mwa Sudan liliua watu 21 na kujeruhi wengine 67 Jumapili, chanzo cha matibabu kimeiambia AFP, kikilaumu wanamgambo kuhusika na shambulizi hilo.
Watoto 17 wamefariki katika moto ulioteketeza bweni la shule yao ya msingi usiku wa kuamkia Ijumaa, katikati mwa Kenya, polisi ilisema.
Rwanda imemkuta na hatia mzee mwenye umri wa miaka 75 kwa kushiriki katika mauaji ya kimbari ya 1994, na kumuhukumu miaka 20 jela, chombo cha habari kinachoungwa mkono na serikali kiliripoti Alhamisi.
Shehena ya kwanza ya dozi 100,000 za chanjo ya mpox itawasili nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Alhamisi, kituo cha kudhibiti na kuzuia magonjwa barani Afrika kimesema, huku jumla ya chanjo 200,000 zikitarajiwa wiki hii.
Zoezi la serikali ya Namibia la kukusanya zaidi ya wanyapori 700 kukabiliana na ukame mbaya zaidi katika miongo kadhaa linaendelea, huku takriban wanyama 160 wakiwa tayari wameuawa, wizara ya mazingira ilisema Jumanne.
Mpinzani maarufu wa Uganda, Bobi Wine, alipigwa risasi kwenye mguu na polisi Jumanne katikati mwa nchi, imetangazwa katika ujumbe kwenye akaunti yake rasmi kwenye mtandao wa kijamii wa X.
Mahakama ya Tunisia ilisema Ijumaa kwamba imekubali rufaa ya mgombea urais ambaye uteuzi wake ulikuwa umekataliwa, na hivyo kumruhusu kugombea katika uchaguzi wa Oktoba 6.
Mahakama moja nchini Algeria Alhamisi ilimuachilia mpinzani mashuhuri Fethi Ghares na mke wake chini ya ufuatiliaji wa mahakama wakati uchunguzi kuhusu madai ya kumtusi Rais Abdelmadjid Tebboune na kuhusu mashtaka mengine ukiendelea, wakili wake alisema.
Rais wa Senegal Bassirou Diomaye Faye Alhamisi aliomba msaada zaidi wa Umoja wa Ulaya katika kukabiliana na ukosefu wa usalama katika kanda ya Sahel wakati waziri mkuu wa Uhispania Pedro Sanchez akikamilisha ziara yake huko Afrika Magharibi.
Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Jumatano liliiambia AFP kwamba mateka wa zamani 43 wa kundi la ADF lenye uhusiano la Islamic State waliookolewa na majeshi ya Congo na Uganda wamerejea katika maisha ya kawaida.
Uhispania ilisaini mikataba na Mauritania na Gambia kuimarisha ushirikiano katika kukabiliana na usafirishaji haramu wa watu na kudumisha uhamiaji halali.
Mvua kubwa zilizonyesha nchini India zimesababisha mafuriko makubwa na vifo vya takriban watu 15, vyombo vya habari vya ndani viliripoti leo Jumatano.
Senegal ilisema Jumanne kwamba imesimamisha kwa muda shughuli za uchimbaji madini kwenye ukingo wa mto ambao ni sehemu ya mpaka wake wa kusini mashariki na Mali, kwa lengo la kuhifadhi mazingira na kulinda afya ya wenyeji.
Waendesha mashtaka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Jumanne waliomba washtakiwa 50 kufikishwa mahakamani na kukabiliwa na adhabu ya kifo kutokana na kile jeshi linasema ni kushiriki katika jaribio la mapinduzi.
Pandisha zaidi