Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 09:50

EU yatoa msaada wa euro milioni 5.4 kwa nchi za Afrika Magharibi zilizokumbwa na mafuriko


Nyumba zilizozama ndani ya maji baada ya mafuriko makubwa mjini N'djamena, Oktoba 14, 2022.
Nyumba zilizozama ndani ya maji baada ya mafuriko makubwa mjini N'djamena, Oktoba 14, 2022.

Umoja wa Ulaya ulitoa msaada wa euro milioni 5.4 kwa nchi sita za Afrika Magharibi na Afrika ya Kati zilizokumbwa na mafuriko mabaya, ujumbe wa Umoja wa Ulaya nchini Chad ulisema Jumatano.

Msaada huo wa kibinadamu utawasaidia watu walioathiriwa zaidi kufuatia mafuriko makubwa nchini Chad, Niger, Nigeria, Cameroon, Mali na Burkina Faso,” ujumbe huo ulisema katika taarifa.

Tangu msimu wa mvua uanze, mvua kubwa iliteketeza majimbo kadhaa.

Kufikia sasa, mvua hiyo imesababisha vifo vya zaidi ya watu 1,500, na kuathiri watu milioni nne na wengine milioni 1.2 wamelazimika kuhama makazi yao katika nchi hizo sita pamoja na Guinea, kulingana na shirika la kimataifa la uhamiaji (IOM).

“Mafuriko ya mwaka huu hayajawahi kutokea, ni ukumbusho mkubwa wa athari zinazoongezeka za mabadiliko ya hali ya hewa katika kanda yetu,” alisema Sylvia Ekra, mkurugenzi wa IOM kanda ya Afrika Magharibi na Kati.

Mfuko huo wa Umoja wa Ulaya umetenga euro milioni 1.35 kwa Niger, euro milioni 1.1 kwa Nigeria, euro milioni 1 kwa Chad na Mali kila moja, euro 650,000 kwa Cameroon na euro 350,000 kwa Burkina Faso.

Forum

XS
SM
MD
LG