Mamlaka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Jumatatu ilielezea masikitiko yake juu ya kitendo cha kushambuliwa kwa wanadiplomasia watatu wa Ufaransa katika mji mkuu Kinshasa, vyanzo vya serikali na kidiplomasia viliiambia AFP.
Watu 132 walifariki mwaka huu katika nchi ya Sudan inayokumbwa na vita kutokana na mafuriko yaliyosbabishwa na mvua kubwa, wizara ya afya ilisema Jumatatu.
Rais wa Tunisia Kais Saied Jumapili alibadilisha mawaziri wengi, akiwemo wa wizara ya mambo ya nje na ulinzi, ofisi ya rais wa Tunisia ilisema katika taarifa iliyochapishwa kwenye mtandao wa Facebook bila maelezo.
Mamlaka ya usafiri wa anga ya Somalia imetishia kusimamisha safari zote za ndege za shirika la ndege la Ethiopia kuelekea nchini humo, vyombo vya habari vya serikali vilisema Jumatano, kitendo cha hivi karibuni katika mzozo wa muda mrefu unaohusu jimbo la Somaliland lililojitenga.
Mfalme wa Morocco Mohammed wa Sita aliwasamehe zaidi ya wakulima 4,800 wanaoshtumiwa kulima bangi kinyume cha sheria, wizara ya sheria ilisema Jumatatu.
Watu 7 wakiwemo watoto wanne walifariki mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo baada ya watu wenye silaha kushambulia lori la mafuta, vyanzo vya eneo hilo viliiambia AFP Alhamisi.
Mafuriko katika jimbo la kaskazini mashariki mwa Chad la Tibesti yaliua watu 54, maafisa walisema.
Marekani Jumatano ilisema “imeshtushwa” na ripoti kwamba polisi wa Tanzania walitumia nguvu kupita kiasi walipowakamata wanachama kadhaa wa upinzani kutokana na mkutano wa vijana uliopigwa marufuku wiki hii.
Mamia ya Watunisia waliandamana Jumanne katika mji mkuu Tunis, wakiadhimisha siku ya kitaifa ya wanawake na kuomba kuachiliwa kwa wanawake wanaoshikiliwa kwa kumkosoa Rais Kais Saied, ripota wa AFP ameshuhudia maandamano hayo.
Chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania, Chadema Jumanne kilidai kwamba viongozi wake kadhaa walipigwa wakati wa kamata kamata ya watu wengi kabla ya mkutano uliopigwa marufuku.
Chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania Jumatatu kimeomba kuachiliwa kwa viongozi wake wakuu ambao walishikiliwa katika kamata kamata ya watu wengi kabla ya mkutano wa hadhara wa siku ya vijana uliopigwa marufuku.
Rais wa Rwanda Paul Kagame alikula kiapo Jumapili kwa muhula wa nne, akisema amani ya kikanda ni “kipaumbele chake” katika kukabiliana na mzozo unaoendelea katika nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Polisi wa Tanzania Jumapili walipiga maarufuku mkutano uliokuwa umepangwa wa vijana wa chama kikuu cha upinzani, Chadema, wakiwatuhumu kupanga maandamano yenye vurugu.
Rais wa Russia Vladimir Putin amefanya kikao na wanachama wa kudumu wa baraza la usalama, na kujadili namna ya kupambana na ugaidi, wakati wanajeshi wa Russia wanapambana na wanajeshi wa Ukraine mpakani.
Wanajeshi wa mwisho wa Marekani waliondoka Jumatatu katika kambi yao nchini Niger, zaidi ya mwaka mmoja baada ya viongozi wa mapinduzi kuwataka kuondoka.
Mali Jumapili ilisema imevunja uhusiano wa kidiplomasia na Ukraine, ikimshtumu afisa mkuu wa Ukraine kuwa alikiri kuhusika kwa Kyiv katika kipigo kibaya walichopata wanajeshi wa Mali mwezi Julai katika mapigano kati yao na waasi wanaotaka kujitenga na wanajihadi.
Polisi wa Zimbabwe wamewafungulia mashtaka wanaharakati 18 walioshiriki maandamano ya kutaka kiongozi mkuu wa upinzani aachiliwe huru, huku serikali ikionya kukabiliana na maandamano kabla ya mkutano wa kikanda.
Waasi wanaotaka kujitenga kaskazini mwa Mali Alhamisi walisema waliwaua wapiganaji kadhaa wa kundi la mamluki wa Russia la Wagner na wanajeshi wa serikali karibu na mpaka wa Algeria mwishoni mwa mwezi Julai.
Ubadilishanaji wa wafungwa wa kihistoria kati ya Marekani na Russia ambao umepelekea kuachiliwa kwa mwandishi wa habari Evan Gershkovich na raia 15 wa nchi za Magharibi ni matunda ya mazungumzo magumu ya siri.
Mahakama nchini Guinea Jumatano ilimuhukumu kiongozi wa zamani dikteta Moussa Dadis Camara kifungo cha miaka 20 jela kwa uhalifu dhidi ya ubinadamu, baada ya kesi ya kihistoria kuhusu mauaji ya mwaka 2009 katika mkutano wa kisiasa.
Pandisha zaidi