Baada ya wanajeshi 800 kuondoka kambini katika mji mkuu wa Niamey mapema mwezi Julai, takriban wanajeshi 200 walibaki katika kambi kubwa ya Agadez kaskazini mwa Niger.
Mchakato wa kuwaondoa wanajeshi wa Marekani na vifaa vyao katika uwanja wa kijeshi huko Agadez umekamilika,” wizara ya ulinzi wa Marekani (Pentagon) ilisema katika taarifa ya pamoja na wizara ya ulinzi wa Niger.
Naibu msemaji wa wizara ya ulinzi Sabrina Singh aliwaambia waandishi wa habari kwamba “chini ya wanajeshi 20” bado wako uwanjani nchini Niger.
Alisema waliobaki wapo kwenye ubalozi wa Marekani na wanaendelea na shughuli za utawala wakijiandaa kwa ajili ya kukamilisha zoezi la kuondoka.”
Tovuti ya Niger Air-info news ilithibitisha kuondoka kwa wanajeshi wa mwisho kutoka Agadez.
Ilisema maafisa kutoka nchi zote mbili walihudhuria hafla ya makabidhiano, ambayo ilimalizika kwa kupaa kwa ndege ya mwisho ya jeshi la Marekani.
Forum