Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 09:31

Marekani na Russia zafanya ubadilishanaji wa wafungwa wa kihistoria


Biden akiwa na familia za wafungwa wa Marekani walioachiliwa na Russia, kwenye White House, Agosti 1, 2024. Picha ya AFP
Biden akiwa na familia za wafungwa wa Marekani walioachiliwa na Russia, kwenye White House, Agosti 1, 2024. Picha ya AFP

Ubadilishanaji wa wafungwa wa kihistoria kati ya Marekani na Russia ambao umepelekea kuachiliwa kwa mwandishi wa habari Evan Gershkovich na raia 15 wa nchi za Magharibi ni matunda ya mazungumzo magumu ya siri.

Warussia wanane waliokuwa wanazuiliwa jela hapa Marekani, Ujerumani, Poland, Norway na Slovania waliachiliwa pia katika ubalishanaji huo.

Biden Alhamisi alizikaribisha kwenye White House familia za raia watatu wa Marekani na mkazi wa kudumu hapa Marekani, wakati zoezi la kuwaachilia wafungwa hao likifanyika mjini Ankara, Uturuki.

Baada ya kuzungumza kwa simu na wapendwa wao kwenye ofisi ya rais, walionekana wakiwa na rais mbele ya waandishi wa habari.

Akiulizwa alichowambia Wamarekani hao walioachiwa huru, Biden alijibu “Nimesema, “Karibuni nyumbani.”

White House ilifanya kazi kwa bidi na muda mrefu kwa siri, ili mwanahabari wa Gazeti la Wall Street Journal, mwanajeshi wa zamani wa Marekani Paul Whelan, ripota wa Radio Liberty Alsi Kurmasheva, na mkazi wa kudumu wa hapa Marekani Vladimir Kara Murza, mkosoaji wa Putin waweze kuachiliwa.

Forum

XS
SM
MD
LG