Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Novemba 14, 2024 Local time: 23:28

Watu 132 wafariki mwaka huu nchini Sudan kutokana na mafuriko


Nyumba zikizungukwa na mafuriko katika kijiji kilicho karibu na mji wa Meroe, nchini Sudan, Agosti 7, 2023. Picha ya AP
Nyumba zikizungukwa na mafuriko katika kijiji kilicho karibu na mji wa Meroe, nchini Sudan, Agosti 7, 2023. Picha ya AP

Watu 132 walifariki mwaka huu katika nchi ya Sudan inayokumbwa na vita kutokana na mafuriko yaliyosbabishwa na mvua kubwa, wizara ya afya ilisema Jumatatu.

Nchi hiyo imekumbwa na msimu wa mvua nyingi tangu mwezi uliopita, huku mafuriko ya hapa na pale yakitokea hasa kaskazini na mashariki mwa nchi.

Wizara hiyo ilisema katika taarifa “Idadi ya jumla ya majimbo yaliyoathiriwa ni 10, huku idadi ya familia zilizoathiriwa ikiongezeka hadi familia 31,666 na watu wengine wapatao 129, 650.”

Imeongeza kuwa idadi ya jumla ya vifo ni 132.

Wakati mafuriko yakitokea kila mwaka nchini Sudan, athari inatarajiwa kuwa mbaya mwaka huu baada ya zaidi ya miezi 16 ya mapigano kati ya majenerali hasimu ambayo yalisababisha mamilioni ya watu kuhama makazi yao na kuishi katika maeneo yenye mafuriko.

Zaidi ya nyumba 12,000 zilibomoka kabisa na nyingine 11,472 zilibomoka kwa kiasi kutokana na mvua hiyo, kulingana na wizara ya afya, ambayo ilisema uharibifu mkubwa ulitokea katika majimbo ya Kaskazini na River Nile.

Forum

XS
SM
MD
LG