Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 20:42

Putin akutana na Baraza la Usalama na kujadili namna ya kupambana na ugaidi

Rais Vladimir Putin (kulia) akiongoza kikao cha wanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama kuhusu hali ilivyo katika mkoa wa Kursk, nyumbani kwake nje ya mji wa Moscow Agosti 9, 2024. (Picha na shirika la habari la serikali la Sputnik}

Ukraine imeendelea kutekeleza mashambulizi mpakani, ikishambulia Russia kufikia leo Ijumaa.

Wanajeshi wa Ukraine vile vile wametekeleza mashambulizi kadhaa ya anga dhidi ya kiwanja cha ndege cha Russia, mamia ya kilomita kutoka mstari wa mbele.

Mashambulizi ya Ukraine dhidi ya Kursk, ndani ya Russia, yalianza jumanne, na yanaonekana kuwa makubwa ndani ya Russia, tangu Moscow ilipovamia Ukraine, Februari mwaka 2022.

Russia imesema kwamba karibu wanajeshi 1000 wa Ukraine na zaidi ya darzeni ya magari ya vita yanahusika katika mashambulizi hayo.

Russia imesema imeharibu silaha na magari kadhaa ya Ukraine.

Ukraine haijasema wazi iwapo inahusika na oparesheni hiyo lakini rais Volodymyr Zelensky alisema alhamisi jioni kwamba Russia ilihitaji kuhisi uchungu wa uvamizi wake.

Forum

XS
SM
MD
LG