Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 09:58

Ukraine na Russia zapambana katika eleo la mpakani


Vikosi vya Russia na Ukraine vinapambana katika eneo la Kursk, Russia kwa siku ya tatu mfululizo, Wizara ya Ulinzi ya Russia imesema Alhamisi.

Russia imeelezea kama moja ya uvamizi mkubwa zaidi wa mpaka wa vikosi vya Ukraine wakati wa vita vilivyoanza miaka miwili na nusu mpaka sasa na uvamizi wa Moscow kwa Ukraine kwenye mpaka wake wa mashariki na Russia.

Lakini taarifa ya Wizara ya Ulinzi imesema wanajeshi wa Russia na walinzi wa mpaka wamezuia vikosi vya Ukraine kuingia ndani zaidi katika eneo la Kursk kusini magharibi mwa Russia.

Imesema jeshi linawashambulia wapiganaji wa Ukraine wanaojaribu kusonga mbele kutoka eneo la Sumy nchini Ukraine.

“Majaribio ya kikosi chochote kusonga ndani zaidi ya kwenda mwelekeo wa Kursk yatazuiliwa,” imesema wizara ya ulinzi.

Forum

XS
SM
MD
LG