Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Septemba 19, 2024 Local time: 08:52

Raia wa Poland wakamatwa Nigeria kwa kupeperusha vibendera vya Russia kwenye maandamano


Picha ya waandamanji wa Nigeria wakilalamikia hali ngumu ya kiuchumi. Agosti 1,2024
Picha ya waandamanji wa Nigeria wakilalamikia hali ngumu ya kiuchumi. Agosti 1,2024

Msemaji wa idara ya  usalama ya jimbo la kaskazini mwa Nigeria la Kano, Peter Afunanya, amesema  Jumatano kuwa Nigeria wiki hii imewakamata raia 7 wa Poland, kwa kupeperusha vibendera vya Russia wakati wa maandamano dhidi ya serikali.

Maelfu ya wanigeria tangu Agosti mosi, wamekuwa wakiandamana dhidi ya mageuzi magumu ya kiuchumi yaliyofanywa na rais Bola Tinubu, ambayo ni kuondoa ruzuku kwenye mafuta na umeme, pamoja na kushusha thamani ya sarafu ya Naira, hali ili yosababisha mfumuko mbaya sana wa bei ndani ya miongo mitatu.

Baadhi ya waandamanaji walibeba vibendera vya Russia wakati wa maandamano hayo hasa kwenye majimbo ya kaskazini, hali inayoashiria kuongezeka kwa ushawishi wa Russia kwenye taifa hilo la Afrika Magharibi.

Mkuu wa jeshi wa Nigeria Jenerali Christopher Musa, ameutaja upeperushaji wa vibendera vya kigeni kwenye maandamano dhidi ya serikali ni ‘kosa la uhaini’, muda mfupi baada ya kufanya kikao na rais Bola Tinubu, siku ya Jumatatu.

Forum

XS
SM
MD
LG