Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 09:18

Polisi Nigeria wako katika hali ya tahadhari


Machafuko nchini Nigeria.
Machafuko nchini Nigeria.

Polisi nchini Nigeria wamekuwa katika hali ya tahadhari leo Ijumaa, na huenda wakaomba msaada  wa wanajeshi, baada ya maandamano kuzua vurugu katika baadhi ya miji.

Pia maandamano hayo yamesababisha vifo vya takriban watu watatu, Inspekta Jenerali wa polisi amesema.

Baadhi ya miji mikubwa, ikiwa ni pamoja na mji mkuu Abuja, na ule wa Kano, ulioko kaskazini mwa nchi, ambapo siku ya Alhamisi ilishuhudia mapambano kati ya polisi na waandamanaji na uporaji, ilionekana kuwa tulivu mapema Ijumaa huku maandamano yakitarajiwa kuendelea.

Wakihamasishwa na maandamano yaliyoongozwa na vijana nchini Kenya, Wanigeria walipanga maandamano, chini ya hashtag '#EndBadGovernanceInNigeria' mtandaoni, wakisema yataendelea kwa siku 10.

Waandamanaji wamekasirishwa na mageuzi ya kiuchumi ya Rais Bola Tinubu ambayo yamesababisha mfumuko mkubwa wa bei, kudhoofisha sarafu na kuwasababishia raia wa kawaida wa Nigeria hali ngumu ya maisha.

Forum

XS
SM
MD
LG