Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Septemba 09, 2024 Local time: 08:58

Watatu wauawa katika maandamano Nigeria


Waandamanaji wakiandamana katika mji mkuu wa Abuja Nigeria Agosti 1, 2024.Picha na Kola Sulaimon / AFP.
Waandamanaji wakiandamana katika mji mkuu wa Abuja Nigeria Agosti 1, 2024.Picha na Kola Sulaimon / AFP.

Takriban waandamanaji watatu wameuawa katika jimbo la Kaduna nchini Nigeria, shirika la habari la Reuters na mashuhuda wamesema, wakati waandamanaji walipoandamana kote katika taifa hilo la Afrika Magharibi dhidi ya kupanda kwa gharama za maisha na masuala ya utawala.

Msemaji wa polisi wa jimbo la Kaduna Mansur Hassan amesema, polisi walitumia gesi ya kutoa machozi na siyo risasi za moto.

Polisi pia waliutawanya umati wa waandamanaji kwa kutumia gesi ya kutoa machozi katika mji mkuu wa Abuja, kulingana na maelezo ya shuhuda.

Wakiwa wamehamasishwa na maandamano ya Kenya mwezi Juni ambayo yalisababisha serikali nchini humo kufuta baadhi ya ongezeko la kodi zilizopangwa,.

Wanigeria wamekuwa wakihamasisha mitandaoni kutaka kurudishwa kwa ruzuku ya mafuta ya petroli na umeme, elimu ya bure kwa shule za msingi na sekondari na kuchukua hatua kupambana na ukosefu wa usalama miongoni mwa madai mengine.

Forum

XS
SM
MD
LG