Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 09:02

Polisi wa Kenya wapiga marufuku maandamano ya kuipinga serikali


Maandamano ya kupinga kuongeza kwa ushuru nchini Kenya, Julai 7, 2024. Picha ya Reuters
Maandamano ya kupinga kuongeza kwa ushuru nchini Kenya, Julai 7, 2024. Picha ya Reuters

Polisi wa Kenya Jumatano walisema “hakuna maandamano yatakayoruhusiwa” Katikati mwa mji mkuu, Nairobi, kufuatia maandamano ya kuipinga serikali, yaliyosababisha vifo.

Nchi hiyo imekumbwa na maandamano yaliyokuwa ya amani hapo awali ambayo yalichochewa na muswada uliotupiliwa mbali wa kuongeza ushuru, na kugeuka maandamano ya vurugu yaliyosababisha vifo vya watu kadhaa, kulingana na kundi la haki za binadamu linalofadhiliwa na serikali.

Rais William Ruto amekabiliwa na changamoto ya kutuliza hali hiyo, kwa kutosaini muswada wa fedha uliopendekeza kuongezwa kwa ushuru, kulivunja baraza la mawaziri na kuahidi kupunguza matumizi ya serikali.

Lakini maandamano ambayo si makubwa ukilinganisha na mwezi uliopita, yaliendelea nchini kote, huku wengi wakimuomba kiongozi huyo wa Kenya kujiuzulu.

“Hakuna maandamano yatakayoruhusiwa katika eneo la biashara Katikati mwa mji wa Nairobi na maeneo mengine yaliyokaribu hadi itakapotolewa taarifa nyingine ili kuhakikisha usalama wa umma,” kaimu mkuu wa polisi wa taifa Douglas Kanja alisema katika taarifa Jumatano jioni.

Eneo hilo lilikuwa kitovu cha maandamano kadhaa ya awali katika mji huo wa Nairobi.

Kabla ya marufuku hiyo, baadhi ya mabango yalikuwa yamesambazwa mtandaoni kuwataka waandamanaji kukusanyika karibu na Uhuru Park kabla ya kuandamana hadi Ikulu leo Alhamisi.

Forum

XS
SM
MD
LG