Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 08:44

Ruto ateua baraza jipya la mawaziri


Rais wa Kenya Wiliiam Ruto.
Rais wa Kenya Wiliiam Ruto.

Rais wa Kenya William Ruto, anayekabiliwa na mzozo, Ijumaa aliteua baraza jipya la mawaziri, huku akianza mchakato wa kuunda serikali ambayo amesema itakuwa "jumuishi."

Katika hotuba kutika ikulu ya Nairobi, iliyopepereushwa moja kwa moja na vyombo vya habari, Ruto alitangaza majina 11 ya mawaziri waliopendekezwa, ikiwa ni pamoja na mwanasheria mkuu, baada ya wiki jana kufukuza karibu baraza lake lote, katika juhudi za kudhibiti mzozo mbaya zaidi wa urais wake wa takriban miaka miwili.

Sita kati ya walioteuliwa, walikuwa katika baraza lake lililovunjwa. Majina hayo yatawasilishwa bungeni ili kuidhinishwa.

Rais huyo amaesema kuwa anaendelea kushauriana na wadau mbalimbali kuhusu baraza hilo.

"Ninaendelea kushauriana na pande zote za kisiasa kuhusu uwiano katika baraza la mawaziri.

Mashauriano yamepiga hatua kubwa, na taratibu za ndani katika sekta mbalimbali zinaendelea ili kuwezesha uteuzi wangu wa uwiano wa baraza hili la mawaziri," alisema.

Forum

XS
SM
MD
LG