Maandamano hayo yamezua mzozo mkubwa zaidi wa miaka miwili ya Ruto mamlakani na yameendelea – japo ni idadi ndogo ya waandamanji waliojitokeza ikilinganishwa na maandamano ya siku za nyuma - hata baada ya rais kuondoa dola bilioni 2.7 katika nyongeza ya kodi iliyokuwa imependekezwa, na kufukuza karibu baraza lake lote la mawaziri.
Waandamanaji wengi wanamtaka Ruto ang'atuke madarakani, wakimlaumu kwa uongozi mbaya, ufisadi na vifo vya dazani za waandamanaji wakati wa maandamano ya awali dhidi ya serikali.
Siku ya Jumanne, polisi walirusha vitoa machozi huko Kitengela, mji ulioko kusini mwa mji mkuu Nairobi, ambapo waandamanaji karibu 200 walichoma matairi na kuimba "Ruto lazima aende" na "Acheni kutuua", waandishi wa habari wa Reuters walisema.
Maandamano hayo yalianza kwa amani lakini baadaye yakageuka kuwa ghasia. Baadhi ya waandamanaji walivamia bunge kwa muda mfupi Juni 25, na polisi walifyatua risasi. Zaidi ya watu 40 wameuawa katika maandamano hayo, mashirika ya kutetea haki za binadamu yanasema.
Ruto Jumatatu alishutumu Ford Foundation, taasisi ya hisani ya Marekani, kwa kufadhili wale waliosababisha "vurugu na ghasia" nchini Kenya, bila kutoa ushahidi.
Tassisi hiyo ilikanusha madai hayo, ikisema haikufadhili maandamano na ina sera ya kutoegemea upande wowote kwa utoaji wake wa ruzuku.
Forum