Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 22:18

Miili ya wanawake inaendelea kupatikana Kware, Nairobi


Bendera ya Kenya
Bendera ya Kenya

Miili mitano zaidi ya watu imepatikana imetupwa katika sehemu ya kutupa taka, katika mtaa wa Mukuru kwa njenga, kitongoji cha Kware, Nairobi Kenya.

Miili hiyo ilikuwa imefungwa ndani ya gunia tofauti. Kuna hofu kwamba huenda idadi ya miili hiyo ikaongezeka.

Idadi imefikia miili kumi kufikia sasa na ilianza kupatikana Ijumaa.

Maafisa wa ujasusi wameendelea kutafuta miili huku wakiomba wakaazi wa sehemu hiyo kuwa wenye subra, uchunguzi ukiendelea.

Polisi wamesema baadhi ya miili ilikuwa imeanza kuoza, na kwamba huenda waliuawa kwingine na miili kutupwa hapo.

Miili yote iliyopatikana kufikia sasa ni wanawake.

Forum

XS
SM
MD
LG