Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 22:02

Polisi wa Kenya waahidi kufanya uchunguzi kuhusu miili minane ya wanawake


map kenya
map kenya

Polisi nchini Kenya Jumapili waliahidi uchunguzi wa “wazi” kuhusu ugunduzi wa kushangaza wa miili minane ya wanawake iliyokatwakatwa na kutupwa katika eneo la taka mjini Nairobi.

Lakini hali ya wasiwasi ilikuwa ikitanda katika eneo la makazi duni la Mukuru kusini mwa mji mkuu wa Kenya, huku polisi wakifyatua mabomu ya kutoa machozi kwa muda mfupi ili kutawanya umati wa wakazi waliokuwa na hasira, mwandishi wa habari wa AFP alisema.

Wakuu wa polisi walisema wanaendelea kuchunguza tukio hilo baya ambalo wanadhani linaweza kuwa na uhusiano na madhehebu, wauaji wenye tabia ya kuua watu wengi au waganga wa kienyeji, na ambalo limelishutusha taifa.

Miili iliyokatwakatwa iliyohifadhiwa katika mifuko ya plastiki, ilitolewa nje ya bahari ya takataka katika eneo ambako hakuna wakazi la Mukuru.

Kaimu mkuu wa polisi ya taifa Douglas Kanja alisema maiti sita zilipatikana huko Mukuru siku ya Ijumaa na viungo zaidi vya mwili vilipatikana Jumamosi, huku uchunguzi wa awali ukionyesha kuwa wote walikuwa wanawake.

“Walikatwa vipande vipande katika hali tofauti ya kuoza na kuachwa ndani ya magunia,” Kanja aliuambia mkutano wa waandishi wa habari, akikielezea kama “kitendo cha kikatili”.

Alisema polisi wana dhamira ya kufanya “uchunguzi wa wazi, wa kina na wa haraka” na kuongeza kuwa wana lengo la kukamilisha uchunguzi wao ndani ya siku 21.

Forum

XS
SM
MD
LG