Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 06, 2024 Local time: 10:08

Nigeria yaipiga  faini kampuni ya Meta dola milioni 220 kwa ukiukaji wa mara nyingi na unaojirudia


Rais wa Nigeria Bola Tinubu baada ya hafla ya kuapishwa kwake mjini Abuja Nigeria May 29, 2023. REUTERS
Rais wa Nigeria Bola Tinubu baada ya hafla ya kuapishwa kwake mjini Abuja Nigeria May 29, 2023. REUTERS

Nigeria imeipiga  faini kampuni ya Meta ya dola milioni 220 ambayo ni kampuni mama ya Facebook na WhatsApp, kwa ukiukaji wa mara nyingi na unaojirudia

Nigeria imeipiga faini kampuni ya Meta ya dola milioni 220 ambayo ni kampuni mama ya Facebook na WhatsApp, kwa ukiukaji wa mara nyingi na unaojirudia.

Tume ya serikali kuu ya Ushindani na Ulinzi wa Wateja (FCCPC) siku ya Ijumaa iliishutumu Meta kwa kukiuka ulinzi wa data wa nchi na sheria za haki za watumiaji kwenye mtandao wa Facebook na WhatsApp.

Afisa mkuu mtendaji wa FCCPC Adamu Abdullahi alisema uchunguzi uliofanywa na tume hiyo kwa kushirikiana na Tume ya Kulinda Data ya Nigeria kati ya Mei 2021 na Desemba 2023 ulionyesha kuwa ilijihusisha na vitendo vya kuingilia watu au watumiaji wa data nchini Nigeria.

Forum

XS
SM
MD
LG