Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 21:08

Maandamano dhidi ya kupanda gharama ya maisha nchini Nigeria yamepungua


Baadhi ya waandamanaji nchini Nigeria
Baadhi ya waandamanaji nchini Nigeria

Maelfu ya watu waliingia mitaani  katika miji mbalimbali ikiwemo mji mkuu Abuja na mji mkuu wa kibiashara Lagos

Maandamano dhidi ya kupanda kwa gharama za maisha nchini Nigeria yamepungua leo Jumatatu wakati watu wachache walijitokeza katika miji mikubwa baada ya vikosi vya usalama kutumia nguvu kuzima maandamano.

Maelfu ya watu waliingia mitaani katika miji mbalimbali ikiwemo mji mkuu Abuja na mji mkuu wa kibiashara Lagos wakitaka iwepo afueni kutokana na hali ngumu yaiuchumi na kusambaa kwa ukosefu wa usalama katika maandamano yaliyoanza Alhamisi wiki iliyopita na yalitarajiwa kuendelea hadi Agosti 10.

Ongezeko la gharama ya maisha lipezua utata Nigeria. Feb. 16, 2024.
Ongezeko la gharama ya maisha lipezua utata Nigeria. Feb. 16, 2024.

Shirika la Amnesty International limesema watu wasiopungua 13 wameuawa katika mapambano na polisi tangu Alhamisi. Polisi wametaja idadi ya vifo ni saba, wakidai baadhi ya vifo vimetokana na ajali na vingine kutokana na kifaa kulipuka.

Forum

XS
SM
MD
LG