Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Januari 05, 2025 Local time: 01:16

Marekani inasema imeshtushwa na nguvu zilizotumiwa na polisi wa Tanzania kuwakamata wapinzani


Viongozi wa Chadema na wanachama wengine wakiandamana kuomba mabadiliko ya katiba, Januari 24, 2024. Picha ya Reuters
Viongozi wa Chadema na wanachama wengine wakiandamana kuomba mabadiliko ya katiba, Januari 24, 2024. Picha ya Reuters

Marekani Jumatano ilisema “imeshtushwa” na ripoti kwamba polisi wa Tanzania walitumia nguvu kupita kiasi walipowakamata wanachama kadhaa wa upinzani kutokana na mkutano wa vijana uliopigwa marufuku wiki hii.

Viongozi wa chama kikuu cha upinzani, Chadema wakiwemo mwenyekiti wa chama Freeman Mbowe na naibu wake Tundu Lissu na wafuasi wao, walikamatwa kabla ya mkutano wa vijana uliokuwa umepangwa kufanyika Jumatatu katika mji wa kusini magharibi wa Mbeya.

Makundi ya haki za binadamu na wapinzani wa serikali walikosoa kukamatwa kwao, wakisema wanahofia inaweza kuwa ishara ya kurejeshwa kwa juhudi za kuutisha upinzani kabla ya uchaguzi wa taifa wa mwaka ujao.

“Tumeshtushwa na ripoti za kuaminika kwamba polisi walitumia nguvu kupita kiasi wakati wa kamata kamata ya hivi karibuni,” Balozi wa Marekani nchini Tanzania alisema katika taarifa.

Aliongeza kuwa “ Majeraha waliyoyapata yamesababisha baadhi ya wanachama wa chama cha upinzani kulazwa hospitali.”

Polisi walisema watu wapatao 520 walikamatwa nchini kote, wakidai kuwa vurugu zilikuwa zimepangwa.

Chadema kinadai viongozi wake wakuu walipigwa wakati wa kukamatwa kwao na kutuhumu polisi kuwatesa.

“Polisi walitumia vifaa vya umeme kuwatesa watu wakati wa kuwakamata,” Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika alisema Jumatano.

Forum

XS
SM
MD
LG