Watoto watano walifariki Jumatano baada ya treni kugongana na basi la shule nchini Afrika Kusini, na kujeruhi wengine 20, wizara ya uchukuzi ilisema katika taarifa.
Mashambulizi ya ndege zisizokuwa na rubani yaliua watu sita Jumanne katika mji wa kaskazini mwa Mali ambako wanajeshi wa Mali na washirika wao wa Russia walipata hasara kubwa katika mapigano ya hivi karibuni na waasi wanaotaka kujitenga, maafisa wa eneo hilo na waasi wameiambia AFP.
Wizara ya mambo ya nje ya Sudan ambayo inalitii jeshi la serikali linalopigana na wanamgambo wa RSF Jumanne ilisema kwamba “inataka majadiliano zaidi” kabla ya kukabili mwaliko wa Marekani juu ya mazungumzo ya kusitisha mapigano.
Mawaziri wa mambo ya nje wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Rwanda wamefikia makubaliano ya kusitisha mapigano kuanzia Agosti 4 katika mkutano uliofanyika mjini Luanda chini ya upatanishi wa Rais wa Angola, ofisi ya Rais wa Angola ilisema Jumanne.
Ethiopia yenye matatizo ya fedha Jumatatu ilipunguza viwango vya ubadilishaji wa fedha za kigeni kama sehemu ya mpango mpana wa mageuzi ya kiuchumi, huku shirika la kimataifa la fedha (IMF) likiidhinisha mkopo kwa taifa hilo ambalo linatafuta mabilioni ya dola, ili kujikwamua kiuchumi.
Takriban watu 65, wengi wao wakiwa watoto waliuawa tangu siku ya Jumamosi katika mashambulizi ya mabomu yaliyofanywa na wanamgambo wa kikosi cha Rapid Support Forces (RSF) katika mji wa jimbo la Darfur wa El-Fasher, wanaharakati wamesema.
Watu 19 walikufa maji wakati boti yao ilipozama Jumamosi kwenye mto katika jimbo la kaskazini la Amhara nchini Ethiopia, chombo cha habari cha serikali katika jimbo hilo kilisema Jumapili.
Kamati ya nidhamu ya chama tawala nchini Afrika Kusini cha ANC iliamua kumfukuza rais wa zamani Jacob Zuma kwa kuongoza kundi hasimu katika uchaguzi wa Mei, vyombo kadhaa vya habari viliripoti Jumapili.
Ufaransa inajiandaa kukaribisha zaidi ya viongozi 100 wakiwemo wakuu wa nchi na serikali, wafalme pamoja na mke wa Rais wa Marekani Jill Biden kwa ajili ya michezo ya Olympics ya majira ya joto yanayoanza kwa sherehe kubwa kwenye mto Seine siku ya Ijumaa.
Watu kadhaa ambao walijiunga na maandamano ya kupinga ufisadi yaliyozimwa katika mji mkuu wa Uganda Kampala kwa kukaidi marufuku rasmi walifunguliwa mashtaka Jumanne na kuwekwa rumande, mawakili wao wamesema.
Watu 55 walifariki Jumatatu katika maporomoko ya ardhi katika eneo la mbali la Kusini mwa Ethiopia, maafisa wa eneo hilo wamesema, wakionya kwamba idadi ya vifo inaweza kuongezeka.
Kiongozi wa upinzani wa Kenya Raila Odinga Jumapili amesema kuwa haki ndicho kiungo muhimu kueleleka mazungumzo ya aina yoyote yale na serikali kufuatia ghasia ambazo zimeendelea kushuhudiwa, wakati rais William Ruto akionya kuwa ghasia hizo huenda zikasabaratisha nchi.
Rais wa Kenya William Ruto, anayekabiliwa na mzozo, Ijumaa aliteua baraza jipya la mawaziri, huku akianza mchakato wa kuunda serikali ambayo amesema itakuwa "jumuishi."
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amesisitiza dhamira ya serikali yake mpya ya ushirika kukuza uchumi, kubuni nafasi za ajira na kupunguza umaskini alipokuwa anafungua kikao cha bunge Alhamisi, kufuatia uchaguzi wa kwanza ambapo chama chake tawala cha ANC kilipoteza wingi wa kura.
Meya wa Paris, Anne Hidalgo, aliogelea katika maji yenye matope ya Seine Jumatano kuonyesha kuwa mto huo hivi sasa ni msafi kabisa kwa ajili ya matukio ya kuogelea wakati wa michezo ya Olimpiki.
Polisi wa Kenya Jumatano walisema “hakuna maandamano yatakayoruhusiwa” Katikati mwa mji mkuu, Nairobi, kufuatia maandamano ya kuipinga serikali, yaliyosababisha vifo.
Mashirika ya Umoja wa Mataifa na makundi mengine ya kimataifa ya misaada “ nilazima yarudi na kuwasaidia zaidi wananchi wa Sudan”, kiongozi wa shirika la hisani la Madaktari Wasiokuwa na mipaka (MSF) alisema Jumanne.
Watu sita wakiwemo Wapakistani wanne waliuawa na wengine 30 kujeruhiwa katika shambulio la bunduki karibu na msikiti wa Washia katika mji mkuu wa Oman Muscat, maafisa walisema Jumanne, likiwa shambulio nadra katika nchi hiyo ambalo kundi la Islamic State limedai kuhusika.
Wabunge wa Gambia Jumatatu waliidhinisha marufuku ya mwaka 2015 dhidi ya ukeketaji licha ya shinikizo kutoka watu wenye mila za kidini katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi, wakitupilia mbali mswada huo wenye utata unaotaka kubatilisha sheria hiyo baada ya miezi kadhaa ya mjadala mkali.
Polisi nchini Kenya Jumapili waliahidi uchunguzi wa “wazi” kuhusu ugunduzi wa kushangaza wa miili minane ya wanawake iliyokatwakatwa na kutupwa katika eneo la taka mjini Nairobi.
Pandisha zaidi