Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 19:26

Rwanda na DRC zakubaliana kusitisha mapigano mashariki mwa Congo


Rais wa Rwanda Paul Kagame, Rais Joao Lourenco wa Angola na Rais Felix Thisekedi wa DRC wakati wa mkutano wao mjini Luanda, Julai 6, 2022. Picha ya AFP
Rais wa Rwanda Paul Kagame, Rais Joao Lourenco wa Angola na Rais Felix Thisekedi wa DRC wakati wa mkutano wao mjini Luanda, Julai 6, 2022. Picha ya AFP

Mawaziri wa mambo ya nje wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Rwanda wamefikia makubaliano ya kusitisha mapigano kuanzia Agosti 4 katika mkutano uliofanyika mjini Luanda chini ya upatanishi wa Rais wa Angola, ofisi ya Rais wa Angola ilisema Jumanne.

Angola imekuwa mpatanishi katika mzozo mashariki mwa DRC katika jimbo la Kivu Kaskazini, ambapo waasi wa M23 wamekuwa wakipambana na jeshi la Congo tangu mwishoni mwa 2021.

“Mkutano wa mawaziri kati ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Jamhuri ya Rwanda, uliofanyika leo (Jumanne) mjini Luanda chini ya upatanishi wa Jamhuri ya Angola, umekubaliana kuanzishwa kwa mchakato wa kusitisha mapigano utakaonza kutetekelezwa kuanzia saa sita usiku tarehe 4 Agosti,” ofisi ya rais wa Angola ilisema.

Sitisho hilo la mapigano litafuatiliwa na kamati maalum ya kufuatilia uheshimishwaji wa makubaliano hayo, ofisi hiyo ilisema.

Hakuna maelezo zaidi yaliyotolewa.

Makubaliano hayo yanafuatia mkutano kati ya mawaziri wa mambo ya nje wa Rwanda na DRC uliosimamiwa na Rais wa Angola Joao Lourenco kwenye Ikulu katika mji mkuu wa Angola.

Mkutano huo umejiri wakati mkataba wa kusitisha mapigano kati ya waasi wa M23 na wanajeshi wa serikali ya Congo kwa ajili ya kuruhusu utoaji wa misaada ya kibinadamu, muda wake wa utekelezaji ukitarajiwa kumalizika saa tano na dakika 59 usiku tarehe 3 Agosti.

Forum

XS
SM
MD
LG