Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 00:57

Ramaphosa anasema serikali yake ina dhamira ya kukuza uchumi na kupunguza umaskini


Rais Cyril Ramaphosa
Rais Cyril Ramaphosa

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amesisitiza dhamira ya serikali yake mpya ya ushirika kukuza uchumi, kubuni nafasi za ajira na kupunguza umaskini alipokuwa anafungua kikao cha bunge Alhamisi, kufuatia uchaguzi wa kwanza ambapo chama chake tawala cha ANC kilipoteza wingi wa kura.

Akikihutubia kikao cha pamoja cha mabaraza mawili ya bunge baada ya hafla ya uzinduzi, Ramaphosa alitaja pia kati ya vipaumbele vingine kukabiliana na gharama ghali ya maisha na kupunguza uzembe miongoni mwa malengo ya utawala wake.

“Tunadhamira ya kuboresha ustawi wa nchi yetu na wananchi wake kupitia ukuaji shirikishi, kubuni nafasi za ajira na kupunguza umaskini,” rais aliwambia wabunge mjini Cape Town.

Chama cha Ramaphosa cha African National Congress (ANC) kililazimika kufanya muungano na vyama vingine tisa baada ya uchaguzi wa mwezi Mei, kwa kushindwa kupata wingi wa wabunge kwa mara ya kwanza tangu ujio wa demokrasia mwaka 1994.

Kikipoteza sifa kutokana na kashfa za rushwa na rekodi mbovu ya uchumi, chama hicho ambacho kiliongoza vita dhidi ya ubaguzi wa rangi kilipata tu asilimia 40 ya kura.

Forum

XS
SM
MD
LG