Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Agosti 24, 2024 Local time: 01:37

Wabunge wa Gambia waidhinisha marufuku ya ukeketaji wa wanawake


Mwandamanaji anayepinga ukeketaji akishikilia bango nje ya Bunge la Gambia mjini Banjul, Machi 18, 2024. Picha ya AFP
Mwandamanaji anayepinga ukeketaji akishikilia bango nje ya Bunge la Gambia mjini Banjul, Machi 18, 2024. Picha ya AFP

Wabunge wa Gambia Jumatatu waliidhinisha marufuku ya mwaka 2015 dhidi ya ukeketaji licha ya shinikizo kutoka watu wenye mila za kidini katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi, wakitupilia mbali mswada huo wenye utata unaotaka kubatilisha sheria hiyo baada ya miezi kadhaa ya mjadala mkali.

Makundi ya kimataifa ya haki za binadamu na Umoja wa Mataifa waliwaomba wabunge kutupilia mbali mswada huo, wakisema unatishia mafanikio ya miaka kadhaa na ungeifanya Gambia kuwa nchi ya kwanza kubatilisha mafuruku ya ukeketaji wa wanawake.

Wabunge walitupilia mbali rasimu ya sheria hiyo kwa kupiga kura dhidi ya vifungu vyake vyote vilivyopendekezwa.

“Mswada wa marekebisho ya sheria ya Wanawake ya mwaka 2024, baada ya kupitia hatua ya kuzingatiwa na vifungu vyote kupigiwa kura, umekataliwa,” alisema Fabakary Tombong Jatta, Spika wa Bunge la Gambia, akiongeza kuwa mchakato wa kutunga sheria “umekwisha”.

Wanaharakati wanaopinga ukeketaji walicheza na kuimba nje ya bunge baada ya mswada huo kukataliwa, mwanaharakati Absa Samba aliiambia AFP kwa njia ya simu.

Forum

XS
SM
MD
LG