Ajali hiyo ilitokea nyakati za alasiri karibu na kijiji cha Mafube, karibu na mji wa Middelburg, umbali wa kilomita 180 kaskazini mashariki mwa Johannesburg, kulingana na vyombo vya habari vya ndani.
Serikali ilithibitisha katika taarifa “ Ajali mbaya kwenye njia ya kivuko, ilihusisha basi na treni. Ilisababisha vifo vya watoto watano na wengine 20 kujeruhiwa.”
Naibu waziri wa uchukuzi Mkhuleto Hlengwa alisema “ Usalama wa watoto wetu ni muhimu na ni jambo la kushtusha kushuhudia maafa hayo.”
Polisi waliripoti kwamba dereva wa basi hiyo alitoroka eneo la tukio baada ya ajali hiyo, wizara ya uchukuzi ilisema.
Forum