Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 08:18

Jeshi la Mali na wapiganaji wa Russia watuhumiwa kuua watu sita kaskazini mwa Mali


Ramani ya Mali
Ramani ya Mali

Mashambulizi ya ndege zisizokuwa na rubani yaliua watu sita Jumanne katika mji wa kaskazini mwa Mali ambako wanajeshi wa Mali na washirika wao wa Russia walipata hasara kubwa katika mapigano ya hivi karibuni na waasi wanaotaka kujitenga, maafisa wa eneo hilo na waasi wameiambia AFP.

“Ndege hizo zisizokuwa na rubani ziliua raia sita Jumanne, miongoni mwao ni Wasudan, Waniger na Wachad,” afisa mmoja wa eneo hilo alisema baada ya shambulio kwenye mji wa Tinzaouatene karibu na mpaka wa Algeria.

Afisa mwingine ameshtumu wanajeshi wa Mali na wapiganaji wa Russia kuua watu 10 katika shambulio hilo.

Msemaji wa waasi wanaotaka kujitenga Mohamed Elmaouloud aliiambia AFP kwamba “ drone iliyorushwa na jeshi la Mali wakishirikiana na wapiganaji wa Russia wa kundi la Wagner waliwalenga wachimba migodi raia wanaofanya kazi kwenye mgodi karibu na mpaka wa Algeria.

Chanzo kimoja cha Mali kimeiambia AFP kwamba “drones hizo zililenga na kushambulia gari lililokuwa likisafirisha magaidi na silaha zao”, bila kutoa maelezo zaidi.

Jeshi la Mali na Kundi la Wagner walikiri kushindwa vibaya katika eneo hilo siku ya Jumamosi, na kupata hasara kubwa katika mapigano dhidi ya waasi wanaotaka kujitenga na wanajihadi.

Forum

XS
SM
MD
LG