Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 20:05

Watu 19 wakufa maji katika ajali ya boti kaskazini mwa Ethiopia


Ramani ya Ethiopia
Ramani ya Ethiopia

Watu 19 walikufa maji wakati boti yao ilipozama Jumamosi kwenye mto katika jimbo la kaskazini la Amhara nchini Ethiopia, chombo cha habari cha serikali katika jimbo hilo kilisema Jumapili.

“Watu 7 akiwemo mtoto waliokolewa katika mazingira magumu,” the Amhara Media Corporation (AMC) kiliongeza, kikimnuku kiongozi wa eneo hilo.

Boti hiyo ilikuwa ikivusha abiria kwenye mto Tekeze, unaopita kwenye mpaka wa Ethiopia na Eritrea kabla ya kuvuka hadi nchini Sudan ambapo ni makutanio ya nchi hizo tatu.

Maafisa wamesema watu 26 wanakadiriwa kuwa walikuwa ndani ya boti hiyo wakati ajali ilipotokea nyakati za alasiri siku ya Jumamosi.

Miili miwili pekee ndiyo iipatikana, AMC kimesema, kikiongeza kuwa waliookolewa walipelekwa kwenye hospitali za karibu.

Amhara, jimbo la pili la Ethiopia lenye idadi kubwa ya watu, limekumbwa na miezi kadhaa ya mapigano kati ya jeshi la Ethiopia na wanamgambo wa kabila la Amhara wanaojulikana kama Fano.

Ajali hiyo ni tukio baya la pili nchini Ethiopia katika siku za hivi karibuni. Jumatatu, maporomoko ya ardhi kusini mwa nchi yaliua watu 250.

Forum

XS
SM
MD
LG