Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Septemba 08, 2024 Local time: 18:39

Zuma afukuzwa katika chama cha ANC


Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma akihutubia wafuasi wake nje ya Mahakama kuu ya Johannesburg, Juni 3, 2024. Picha ya AFP
Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma akihutubia wafuasi wake nje ya Mahakama kuu ya Johannesburg, Juni 3, 2024. Picha ya AFP

Kamati ya nidhamu ya chama tawala nchini Afrika Kusini cha ANC iliamua kumfukuza rais wa zamani Jacob Zuma kwa kuongoza kundi hasimu katika uchaguzi wa Mei, vyombo kadhaa vya habari viliripoti Jumapili.

Uamuzi huo ambao haujatangazwa rasmi, ulichukuliwa baada ya kesi za kinidhamu kuanzishwa mwezi huu dhidi ya kiongozi huyo wa zamani ambaye bado ana umaarufu.

“Mwanachama aliyeshtakiwa amefukuzwa katika chama cha ANC,” umesema waraka uliovuja, ambao umeonwa pia na shirika la habari la AFP ambao ni wa tarehe 29 Julai.

“Mwanachama aliyeshtakiwa ana haki ya kukata rufaa kwa kamati ya kitaifa ya nidhamu ya rufaa ndani ya siku 21.”

Chama cha African National Congress kilimsimamisha kiongozi huyo wa zamani aliyokumbwa na kashfa mwezi Januari, mwezi mmoja baada ya kukiunga mkono chama kipya cha uMkhonto weSizwe (MK).

MK kilipunguza kura za ANC katika uchaguzi wa tarehe 29 Mei, na kuchukua nafasi ya tatu kwa asilimia 14.5 za kura.

Zuma hivi sasa anaongoza chama hicho, ambacho kina wabunge 58 katika bunge la taifa lenye viti 400.

ANC kilipata asilimia 40 ya kura katika uchaguzi wa Mei, zikiwa kura chache sana tangu kiingie maradakani miongo mitatu iliyopita kuchukua nafasi ya serikali ya ubaguzi wa rangi.

Ukiacha rufaa iliyofanikiwa dhidi ya uamuzi huo, uanachama wa Zuma katika ANC unaweza kufutwa, vyombo vya habari kadhaa viliripoti. Alijiunga na ANC kupitia tawi la vijana la chama hicho akiwa na umri wa miaka 15 mwaka 1959.

Forum

XS
SM
MD
LG