Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 30, 2024 Local time: 19:25

Jill Biden aalikwa katika sherehe za Olympics huko Paris


Mke wa rais wa Marekani Jill Biden akiwa na mume wake rais Joe Biden huko Delaware Agosti 19, 2020. Picha na Olivier DOULIERY / AFP.
Mke wa rais wa Marekani Jill Biden akiwa na mume wake rais Joe Biden huko Delaware Agosti 19, 2020. Picha na Olivier DOULIERY / AFP.

Ufaransa inajiandaa kukaribisha zaidi ya viongozi 100 wakiwemo wakuu wa nchi na serikali, wafalme pamoja na mke wa Rais wa Marekani Jill Biden kwa ajili ya michezo ya Olympics ya majira ya joto yanayoanza kwa sherehe kubwa kwenye mto Seine siku ya Ijumaa.

Hakuna afisa wa serikali ya Vladimir Putin aliyealikwa kutokana na vita vya Kremlin dhidi ya Ukraine, wakati ujumbe wa Israel utalindwa vikali wakati mvutano ukiendelea kutokana na Israel kuendelea na vita kwenye Ukanda wa Gaza.

“Tuko tayari kuikaribisha dunia” alisema Samuel Ducroquet, balozi wa michezo wa Ufaransa

Russia mshindani mkubwa kwa muda mrefu kwenye michezo ya Olimpik ya majira ya joto, imepigwa marufuku kushuriki michezo ya Paris kutokana na uvamizi wa Putin nchini Ukraine, unaoingia mwaka wa tatu, lakini kikosi kidogo cha wanariadha kitaiwakilisha nchi hiyo.

Ukraine iliyokumbwa na vita haijatangaza kama rais Volodymyr Zelensky atahudhuria sherehe hizo za saa tatu.

Waziri mkuu mpya wa Uingereza Keir Starmer, ambaye ana nia ya kuimarisha uhusiano na Ufaransa, atakuwepo jukwaani kutazama gwaride ka kuvutia litakalofanyika mtoni.

Paris 2024 “ni tukio kubwa kwa Ufaransa lakini pia kwa Uingereza” alisema Menna Rawlings, Balozi wa Uingereza nchini Ufaransa , akiongeza kuwa takribani tiketi 500,000 zimeuzwa Uingereza.

Viongozi wengine wanaotarajiwa kuhudhuria ni pamoja na Kansela wa Ujerumen Olaf Scholz, rais wa Italia Sergio Mattarella na wa Finland Alexander Stubb, pamoja na waziri mkuu wa Ugiriki, Kyriakos Mitsotakis.

Forum

XS
SM
MD
LG