Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 08:56

MSF inayaomba mashirika ya Umoja wa Mataifa kurudi Sudan


Nembo ya shirika la madaktari wasiokuwa na mipaka ( MSF)
Nembo ya shirika la madaktari wasiokuwa na mipaka ( MSF)

Mashirika ya Umoja wa Mataifa na makundi mengine ya kimataifa ya misaada “ nilazima yarudi na kuwasaidia zaidi wananchi wa Sudan”, kiongozi wa shirika la hisani la Madaktari Wasiokuwa na mipaka (MSF) alisema Jumanne.

Mwenyekiti wa MSF International Christos Christou aliiambia AFP kwamba baada ya miezi 15 ya mzozo wa kikatili katika taifa hilo la kaskazini mashariki mwa Afrika, mtu mmoja kati ya watatu wanaojeruhiwa ni wanawake au watoto wenye umri wa chini ya miaka 10.

Vita vilizuka mwezi Aprili mwaka 2023 kati ya jeshi la serikali na kikosi cha wanamgambo cha Rapid Support Forces ( RSF), na kuitumbukiza Sudan katika “moja ya mizozo mibaya ya kibinadamu katika kumbukumbu za hivi karibuni”, kulingana na Umoja wa Mataifa.

Vita hivyo vilisababisha shughuli nyingi za kutoa misaada nchini humo kusitishwa.

Mashirika mengi yamechukua “msimamo wa tahadhari, yakisubiri kuona jinsi mzozo huo utakavyoendelea,” Christou aliiambia AFP akiwa huko Port Sudan.

Alizungumza wakati mazungumzo kati ya mjumbe wa Umoja wa Mataifa na wajumbe kutoka pande zinazopigana yakiendelea mjini Geneva.

Wakati huu ambapo njaa inakita mizizi na vita havionyeshi ishara ya kukoma,” tunaomba mashirika mengine, na hasa ya Umoja wa Mataifa kurudi na kusaidia zaidi,” alisema.

Forum

XS
SM
MD
LG