Wabunge wa Gambia Jumatatu waliidhinisha marufuku ya mwaka 2015 dhidi ya ukeketaji licha ya shinikizo kutoka watu wenye mila za kidini katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi, wakitupilia mbali mswada huo wenye utata unaotaka kubatilisha sheria hiyo baada ya miezi kadhaa ya mjadala mkali.
Polisi nchini Kenya Jumapili waliahidi uchunguzi wa “wazi” kuhusu ugunduzi wa kushangaza wa miili minane ya wanawake iliyokatwakatwa na kutupwa katika eneo la taka mjini Nairobi.
Watu watano waliuawa Jumapili jioni katika mlipuko mkubwa wa bomu lililotegwa ndani ya gari kwenye mgahawa katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu, uliokuwa umejaa mashabiki wa soka wakitizama fainali ya Euro 2024, vyombo vya habari vya ndani vilisema, vikinuku polisi.
Rwanda Jumatatu ilisema “inazingatia” uamuzi wa serikali mpya ya chama cha Labour nchini Uingereza kufuta makubaliano yenye utata ya kuwafukuza wahamiaji wanaotafuta hifadhi nchini humo na kuwahamishia katika taifa hilo la Afrika Mashariki.
Jumuia ya uchumi ya nchi za Afrika Magharibi ECOWAS Jumapili ilionya kwamba kanda hiyo inakabiliwa na “kusambaratika” baada ya watawala wa kijeshi wa Niger, Mali na Burkina Faso kusisitiza msimamo wao wa kutaka jumuia hiyo ivunjwe.
Rais wa Nigeria amependekeza kitita cha dola bilioni 1.3 kukabiliana na kupanda kwa bei na ukosefu wa usalama wa chakula huku nchi hiyo ikipambana na mzozo mbaya wa kiuchumi, waziri wa fedha alisema Alhamisi.
Wahamiaji 89 waliokuwa wanaelekea Ulaya walifariki baada ya boti yao kuzama mapema wiki hii kwenye pwani ya Mauritania, shirika la habari la serikali na afisa wa eneo hilo walisema Alhamisi, huku wengine kadhaa wakipotea.
Shambulio la wanamgambo kwenye mgodi wa dhahabu katika jimbo la Ituri liliwaua raia wanne wa China kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kulingana na vyanzo vya eneo hilo.
Kikosi cha pili cha ujumbe wa polisi wa kimataifa unaoongozwa na Kenya nchini Haiti kitawasili nchini humo katika wiki zijazo, waziri mkuu Garry Conille aliiambia AFP Jumanne.
Rais wa Sierra Leone Julius Maada Bio Jumanne alitia saini sheria inayopiga marufuku ndoa za utotoni katika nchi ambako maelfu ya wasichana wanaolewa kabla ya kufikisha miaka 18.
Jumla ya watu 39 waliuawa katika maandamano dhidi ya serikali nchini Kenya, tume ya kitaifa ya haki za binadamu ilisema Jumatatu, huku wanaharakati wakiongeza juhudi za kuitisha duru nyingine ya maandamano wiki hii.
Mamia ya watu waliandamana Jumapili katika mji mkuu wa Kenya Nairobi, kuwaenzi wale waliofariki katika maandamano ya kuipinga serikali wiki iliyopita, huku Rais William Ruto akisisitiza kwamba, na hapa ninamnukuu: “Sihusiki katika umwagaji damu.”
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa alitangaza serikali yake mpya Jumapili huku upinzani ukipata wizara 12 kati ya 32 kufuatia mazungumzo magumu ya kuunda serikali ya ushirika baada ya chama tawala cha African National Congress kupoteza wingi wa viti bungeni.
Wapiganaji wa M23 wanaoaminika kuungwa mkono na Rwanda wameuteka mji wa kimkakati mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, afisa mmoja aliliambia shirika la habari la AFP Jumamosi, huku maeneo jirani pia yakiangukia mikononi mwa waasi.
Mahakama ya juu nchini Burundi Alhamisi ilithibitisha kifungo cha maisha dhidi ya waziri mkuu wa zamani wa nchi hiyo, Jenerali Alain Guillaume Bunyoni, chanzo cha mahakama kimeliambia shirika la habari la AFP.
Mali imewafunga jela wapinzani 10 wa serikali ya kijeshi, wakiwemo viongozi wa upinzani kwa kuomba nchi kurejeshwa chini ya utawala wa kiraia, mawakili wao waliiambia AFP Jumatatu.
Kikosi cha polisi wa Kenya kitaondoka kuelekea Haiti Juni 25, ili kuongoza Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kukabiliana na magenge, licha ya malalamishi yaliyowasilishwa mahakamani dhidi ya hatua hiyo, vyanzo vya serikali na polisi vimesema Jumapili.
Wadhibiti wawili wa vyombo vya habari nchini Guinea Alhamisi walihukumiwa kifungo cha miezi minane jela baada ya kudai kwamba viongozi wa vyombo vya habari maarufu walikuwa wanapewa hongo na utawala wa kijeshi, wakili wao amesema.
Niger imefuta leseni ya kufanya kazi ya mzalishaji wa mafuta ya nyuklia wa Ufaransa, Orano, katika migodi mikubwa zaidi ya uranium duniani, kampuni hiyo ilisema Alhamisi, katika hatua inayoonyesha wazi mvutano kati ya Ufaransa na utawala wa kijeshi wa nchi hiyo ya Afrika Magharibi.
Wadhibiti wawili wa vyombo vya habari walifikishwa mahakamani nchini Guinea Jumatano baada ya kudai kuwa viongozi wa vyombo vya habari maarufu walihongwa na utawala wa kijeshi.
Pandisha zaidi