Rais wa Guinea Bissau Umaro Sissoco Embalo Jumatano aliliambia shirika la habari la AFP kwamba aliamuru kufungwa kwa sehemu ya mpaka wa nchi yake na Senegal baada ya mapigano makali kuzuka kati ya jamii mbili za Kiislamu.
Wakufunzi kadhaa wa jeshi la Russia waliwasili nchini Burkina Faso kufuatia shambulio la wanajihadi kaskazini mwa nchi hiyo, vyanzo vilisema Jumanne.
China imejibu vikali Jumatatu kauli ya viongozi wa G7 ikiionya Beijing kuacha kupeleka vipuli vya silaha Russia, ikisema kuwa taarifa yao baada ya mkutano “ilikuwa imejaa kiburi, ubaguzi na uongo.”
Polisi wa Zimbabwe walimkamata na kumshtaki kiongozi wa upinzani Jameson Timba na zaidi ya watu wengine 70 kwa kusababisha vurugu wakati wa mkutano binafsi uliofanyika mwishoni mwa juma, wakili wake alisema Jumatatu.
Rais Joe Biden alitumia ujumbe wake wa Eid al-Adha kwa Waislamu kutetea mpango wa kusitisha mapigano huko Gaza unaoungwa mkono na Marekani, akisema Jumapili kuwa ndiyo njia bora ya kuwasaidia raia wanaoteseka kutokana” na ukatili wa vita kati ya Hamas na Israel.”
Wanajeshi sita wa Niger waliokuwa wanalinda bomba la mafuta la nchi jirani ya Benin waliuawa katika shambulio la “majambazi wenye silaha” kusini mwa nchi, jeshi la Niger lilisema Jumapili.
Mamluki raia wa Romania na wanajeshi wawili wa Congo waliuawa, na mwanajeshi mlinda amani wa Umoja wa Mataifa kujeruhiwa katika matukio matatu tofauti mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, vyanzo kadhaa vilisema Jumapili.
Chama cha upinzani nchini Afrika Kusini Inkatha Freedom Party Jumatano kimetangaza kuwa kitashirikiana na chama tawala cha African National Congress (ANC) huku ANC kikijaribu kuunda serikali ya muungano itakayoweza kuongoza baada ya uchaguzi wa Mei 29.
Polisi wa Kenya watapelekwa nchini Haiti kukabiliana na magenge ya uhalifu pengine ndani ya wiki zijazo, rais wa Kenya William Ruto alisema Jumapili, licha ya pingamizi za mahakama ambazo zilichelewesha mchakato huo.
Rais wa Rwanda Paul Kagame atakabiliana na wapinzani wawili katika uchaguzi wa mwezi ujao, kulingana na orodha ya muda ya wagombea urais iliyochapishwa Alhamisi.
Misri imepokea ishara za matumaini kutoka kwa Hamas kuhusu uwezekano wa kusitisha mapigano huko Gaza na kubadilishana wafungwa na mateka na Israel, shirika la Al-Qahera lenye uhusiano na serikali ya Misri lilisema Alhamisi, likinuku chanzo cha ngazi ya juu.
Rais wa Russia Vladimir Putin Jumatano alitoa wito kwa Moscow “kujenga” uhusiano na serikali ya Taliban, wakati ujumbe wa Taliban ukiitembelea Russia.
Ukuaji wa uchumi wa Kenya utapungua hadi asilimia tano mwaka huu baada ya kuimarika sana mwaka 2023, Benki ya Dunia ilisema Jumatano.
Chama tawala nchini Afrika Kusini cha African National Congress (ANC) Jumatano kilisema kimewasiliana na wapinzani ili kuunda serikali ya umoja wa kitaifa, baada ya kushindwa kupata wingi wa kura katika uchaguzi mkuu wa wiki iliyopita.
Viongozi vya vyama vya wafanyakazi nchini Nigeria Jumanne walisitisha mgomo wa nchi nzima kuruhusu mazungumzo ya kuongezewa mshahara, baada ya mgomo wao kudumaza safari za ndege, kufunga mtambo wa umeme nchini kote na kufunga ofisi za umma na shule.
Shirika la kimataifa la mslaba mwekundu limesimamisha utoaji wa msaada wa chakula kwa maelfu ya kaya zilizohamishwa kwenye makazi yao katika eneo moja la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, huku mapigano yakipamba moto na kulazimisha watu kukimbia.
Wachunguzi wa Kenya Jumatatu waligundua miili saba zaidi huku shughuli ya kufukua miili zaidi ikianza tena katika msitu ambako mamia ya watu waliokufa kwa njaa walizikwa katika makaburi ya pamoja, polisi walisema.
Tehran imemuita balozi mdogo wa muda wa Sweden juu ya “tuhuma zisizokuwa na msingi na za chuki,” wizara ya mambo ya nje ilisema Jumapili, baada ya idara ya ujasusi ya Sweden kusema kuwa Iran “inatumia mitandao ya uhalifu” ndani ya taifa hilo la Scandinavia kuishambulia Israel na maslahi yake.
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa Jumapili aliwataka viongozi wa vyama vya Afrika Kusini kufanya kazi pamoja kwa maslahi ya umma, baada ya chama chake cha ANC kupoteza wingi wa uongozi wa utawala wake uliodumu miaka 30 katika uchaguzi uliokuwa na ushindani mkali.
Dhahabu ya Afrika yenye thamani ya mabilioni ya dola inauzwa kwa njia ya magendo nje ya bara hilo kila mwaka, nyingi ikipelekwa Dubai kabla ya kusafirishwa kwa njia halali kwenda nchi nyingine, shirika lisilo la serikali kutoka Uswisi limesema Alhamisi.
Pandisha zaidi