Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 06:53

Shirika la kimataifa la msalaba mwekundu lasimamisha kutoa msaada wa chakula mashariki mwa DRC


Watu wakikimbia mapigano mashariki mwa DRC
Watu wakikimbia mapigano mashariki mwa DRC

Shirika la kimataifa la mslaba mwekundu limesimamisha utoaji wa msaada wa chakula kwa maelfu ya kaya zilizohamishwa kwenye makazi yao katika eneo moja la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, huku mapigano yakipamba moto na kulazimisha watu kukimbia.

Katika siku chache zilizopita, mapigano kati ya waasi wa M23 na jeshi la Congo yalihamia karibu na mji wa kimkakati wa Kanyabayonga wenye wakazi 600,000, ulioko eneo la kaskazini linalokabiliwa na mzozo.

Maelfu ya watu walikimbia kutoka mji huo katika miezi ya karibuni wakiondoka katika makazi yao kutokana na kusonga mbele kwa waasi ambao walianzisha vita katika eneo hilo mwishoni mwa mwaka 2021.

ICRC imesema ilianza kusambaza chakula kwa watu waliokimbia makazi yao huko Kanyabayonga tarehe 24 Mei, lakini wamelazimika kusimamisha kutoa msaada siku sita baadaye.

“Wakikabiliwa na mapigano karibu na maeneo yao, kaya nyingi zimekimbia tena,” taarifa ya ICRC imesema.

“Tuna wasiwasi kuhusu raia hao. Kila wanapokimbia tena, wanajikuta katika hali ya hatari zaidi,” amesema Myriam Favier, mkuu wa ujumbe wa ICRC katika mji mkuu wa jimbo la Kivu Kaskazini wa Goma.

Maelfu ya watu walikimbilia kwa wingi kwenye vijiji vya kaskazini mwa mji wa Kanyabayonga, vyanzo kadhaa vya eneo hilo vimesema.

Forum

XS
SM
MD
LG