Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 03:09

Benki ya dunia inakadiri uchumi wa Kenya utapungua hadi asilimia 5 mwaka huu


Nembo ya Benki ya Dunia
Nembo ya Benki ya Dunia

Ukuaji wa uchumi wa Kenya utapungua hadi asilimia tano mwaka huu baada ya kuimarika sana mwaka 2023, Benki ya Dunia ilisema Jumatano.

Taifa hilo lenye uchumi imara katika ukanda wa Afrika Mashariki limekumbwa na deni kubwa la umma, mfumko wa bei na serikali ya Rais William Ruto ambayo ilikuwa na upungufu wa fedha, iliweka tozo mpya na nyongeza ya kodi.

Benki ya dunia ilisema katika ripoti kwamba wakati uchumi wa Kenya ulikuwa umekua kwa asilimia 5.6 mwaka jana kutoka asilimia 4.9 mwaka 2022, unatarajiwa kupungua hadi asilimia 5 mwaka huu.

Ripoti hiyo imesema kuimarika kwa sekta muhimu ya kilimo pamoja na hali bora ya hewa, kulichangia katika ukuaji wa uchumi mwaka 2023, huku utalii pia ukichangia kwa hali hiyo imara ya uchumi.

Hata hivyo, ripoti hiyo imesema mauzo ya nje ya Kenya hayakuleta faida ya kutosha, ikibaini kuwa “nchi hiyo haijazalisha bidhaa tofauti za kuuza nje katika miaka ya hivi karibuni na ilipoteza uwezo wa kushindana katika masoko inakouza bidhaa zake.”

Ripoti hiyo ya Benki ya dunia imetolewa wiki moja kabla ya serikali ya Ruto ikitarajiwa kuwasilisha bungeni bajeti yake tarehe 13 Juni.

Serikali inakadiria bajeti ya shilingi trilioni 4.25 kwa mwaka wa fedha unaomalizika tarehe 30 Juni 2025, kutoka shilingi trilioni 3.6 mwaka uliopita.

Forum

XS
SM
MD
LG