Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Juni 30, 2024 Local time: 16:23

Wakufunzi wa kijeshi wa Russia wawasili Burkina Faso


Wakufunzi wa kijeshi wa Russia wakitoa mafunzo kwa raia, Disemba 3, 2022. Picha ya Reuters
Wakufunzi wa kijeshi wa Russia wakitoa mafunzo kwa raia, Disemba 3, 2022. Picha ya Reuters

Wakufunzi kadhaa wa jeshi la Russia waliwasili nchini Burkina Faso kufuatia shambulio la wanajihadi kaskazini mwa nchi hiyo, vyanzo vilisema Jumanne.

Baada ya kuchukua madaraka mwezi Septemba mwaka 2022, viongozi wa mapinduzi wa taifa hilo la Afrika Magharibi walifukuza wanajeshi na wanadiplomasia kutoka Ufaransa, mtawala wa zamani wa kikoloni, na kujenga uhusiano na Russia kwa ajili ya msaada wa kijeshi.

“Ndege zilizofanya safari mara mbili zilizokuwemo wakufunzi wa Russia ziliwasili Burkina Faso kutokana na shambulio hilo,” chanzo cha kidiplomasia kutoka nchi ya Afrika kilisema kwa masharti ya kutotajwa jina, na kuongeza kuwa ndege hizo zilisafiri kutokea nchi jirani ya Mali, taifa lingine linaloongozwa na wanajeshi ambalo lilijenga uhusiano wa karibu na Moscow.

Chanzo kingine huru kilithibitisha kuwasili kwa wakufunzi hao.

Waasi wanajihadi wenye uhusiano na Al-Qaeda na Islamic State walianzisha uasi nchini Burkina Faso tangu 2015 ambao umeua maelfu ya watu na kuwahamisha kwenye makazi yao watu milioni 2.

Tarehe 11 Juni, kundi lenye uhusiano na Al-Qaeda lilishambulia eneo la kaskazini mashariki la Mansila na kikosi cha kijeshi kinachopatikana karibu na mpaka na Niger.

Forum

XS
SM
MD
LG