Mabaki ya watu 436 sasa yamefukuliwa katika jangwa la mbali kutoka mji wa pwani wa Bahari ya Hindi wa Malindi, katika tukio baya lililoshtusha Kenya na ulimwengu.
Picha zilizopeperushwa kwenye televisheni ya Kenya zilionyesha mifuko saba ya plastiki ya rangi ya blu ikiwa imepangwa kwenye ardhi katika msitu wa Shakahola kabla ya kuhamishiwa kwenye gari.
“Tulifukua miili saba leo (Jumatatu). Katika kaburi moja, kulikuwemo miili minne na miili mingine mitatu ikizikwa katika sehemu mbalimbali,” Daktari Johansen Oduor, daktari mkuu wa serikali wa kuchunguza maiti aliwambia waandishi wa habari kwenye eneo la tukio.
Alisema “Kuna makaburi 50 yaliyogunduliwa na tutayafukua.”
Paul Ntenghe Mackenzi aliyejitangaza kuwa mchungaji anadaiwa kuwashawishi wafuasi wake kuacha kula hadi wafe ili “wakutane na Yesu ” kabla ya kile alichotabiri kuwa ni mwisho wa dunia mwezi Agosti mwaka jana.
Alikamatwa mwezi Aprili 2023 baada ya miili ya kwanza kugunduliwa katika kile kilichotajwa kama “mauaji ya msiti wa Shakahola”.
Dereva huyo wa zamani wa taxi aliyegeuka nabii alikana mashtaka 191 ya mauaji, kuua bila kukusudia na ugaidi. Alishtakiwa pia kwa mateso ya watoto na ukatili.
Forum