Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 10:46

China yajibu vikali kauli ya viongozi wa G7


Rais wa China Xi Jinping na Rais wa Russia Vladimir Putin
Rais wa China Xi Jinping na Rais wa Russia Vladimir Putin

China imejibu vikali Jumatatu kauli ya viongozi wa G7 ikiionya Beijing kuacha kupeleka vipuli vya silaha Russia, ikisema kuwa taarifa yao baada ya mkutano  “ilikuwa imejaa kiburi, ubaguzi na uongo.”

Wakati viongozi hao walipokutana wiki iliyopita Italia, walizungumzia mahusiano dhaifu ya kibiashara na China na pia ikiangazia mivutano juu ya Ukraine na bahari ya South China ndiyo yalitawala majadiliano.

Tamko hilo lililotolewa mwisho wa mkutano huo Alhamisi liliikosoa China katika masuala haya mengi.

Ilijumuisha tuhuma dhidi ya Beijing ya kupeleka vifaa kwa Russia ambavyo vinaweza kutumika mara kadhaa, ambavyo wamesema vinasaidia katika vita na Ukraine.

Siku ya Jumatatu msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Lin Jian alisema tamko hilo lilikuwa “limeikashifu na kuishambulia China”.

Kikundi cha nchi Saba - ikiwemo Marekani, Japan, Ufaransa, Ujerumani, Canada, Uingereza na Italia – kilikuwa kimelenga a kile walichokiita uvamizi “hatari sana” unaofanywa na China katika Bahari ya South China.

Wasiwasi wa kuongezeka mivutano ya kijeshi kati ya China na majirani zake unaendelea kukua, Jumatatu meli za Ufilipino na China ziligongana karibu na eneo la Second Thomas Shoal, kulingana na Walinzi wa Pwani wa China.

“Tunapinga China kuligeuza eneo kuwa la kijeshi, na kutumia nguvu na vitisho kwenye Bahari ya South China,” ilisema taarifa ya G7, likitumia lugha kali kuliko ile ya mkutano wa mwaka jana huko Japan.

Forum

XS
SM
MD
LG