Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Julai 04, 2024 Local time: 05:06

Mawaziri wa Mambo ya Nje wa G7 kujadili Usalama


Balozi Christoph Heusgen (Photo by Johannes EISELE / AFP)
Balozi Christoph Heusgen (Photo by Johannes EISELE / AFP)

Mawaziri wa Mambo ya Nje wa G7 wanatarajiwa kukutana pembeni ya mkutano wa kila mwaka  wa Usalama Munich mwishoni mwa wiki.

Taarifa hii ni kwa mujibu wa mwenyekiti wa kikundi hicho iliyotolewa Jumatatu, akiongezea kuwa matamshi ya Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump kuhusu NATO ‘kwa hakika’ yatakuwa kwenye ajenda.

Rais wa zamani Donald Trump
Rais wa zamani Donald Trump

Mwenyekiti wa MSC Christoph Heusgen, balozi wa zamani wa Ujerumani kwa Marekani, aliwaambia waandishi wa habari mjini Berlin, wanadiplomasia wa juu wa Marekani, Uingereza, Canada, Ufaransa, Ujerumani, Italy na Japan watakutana na pia kujadili matamshi ya Trump ambaye alisema hatawalinda wanachama wa NATIO kutokana na mashambulizi yajayo ya Russia kama mchango wa nchi hiyo kwa ushirika wa ulinzi utakuwa unalegalega.

Wakati wa mkutano wa kisiasa Jumamosi huko South Carolina, Trump alilalamika kuhusu kile alichokiita “kushindwa’ kulipa ada zao kwa baadhi ya nchi wanachama wa NATO na alikumbushia kile alichosema mawasiliano ya zamani na mkuu wa ‘nchi moja kubwa’ kuhusu shambulizi lililofanywa na Russia kwa nchi kama hizo.

Forum

XS
SM
MD
LG