Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 18:55

Ufaransa inajaribu kuongeza misaada zaidi kwa wakulima wanaoandamana kuomba malipo bora


Wakulima wa Ufaransa watumia matrekta yao kuzorotesha shughuli karibu na uwanja wa ndege wa Roissy Charles de Gaulle, Januari 27, 2024.
Wakulima wa Ufaransa watumia matrekta yao kuzorotesha shughuli karibu na uwanja wa ndege wa Roissy Charles de Gaulle, Januari 27, 2024.

Serikali ya Ufaransa inatizama uwezekano wa kutoa misaada zaidi kwa wakulima wa nchi hiyo, waziri mkuu Gabriel Attal amesema Jumapili, huku maandamano ya nchi nzima kuomba malipo bora na mazingira bora ya maisha yakiendelea bila ishara yoyote kuwa yatasitishwa.

Wakulima nchini Ufaransa, mzalishaji mkubwa wa bidhaa za kilimo katika Umoja wa Ulaya, wanalalamika kwamba wanakabiliwa na ushindani usio wa haki kutoka kwa washindani wao katika nchi zenye sheria nyepesi zaidi.

Ili kuwashinikiza viongozi kusikiliza hoja zao, waliweka vizuizi kwenye barabara kuu wiki iliyopita.

“Tutafikiria hatua zozote nyingine tunazoweza kuchukua kuhusu masuala hayo ya ushindani usio wa haki,” Attal aliwaambia waandishi wa habari.

Siku ya Ijumaa, serikali iliachana na mipango ya kupunguza kwa hatua ruzuku kwa mafuta ya dizeli na kilimo, na kutangaza hatua nyingine za kupunguza changamato za kifedha na kiutawala zinazowakabili wakulima.

Hata hivyo, wakulima wanaomba hatua zaidi. Chama kikuu cha wakulima wa Ufaransa, FNSEA, kimesema kitaendelea na maandamano na vyama vingine vimetishia kuweka vizuizi vya barabarani karibu na mji wa Paris na kwenye soko la chakula la Rungis karibu na mji mkuu.

Forum

XS
SM
MD
LG